Saturday, October 30, 2010


Ligi Kuu England

Man United 2 Spurs 0, Nani afunga goli la ‘Ze Komedi’

Jumamosi, 30 Oktoba 2010 21:56
ChapishaToleo la kuchapisha
MAN_U_LOGONani alifunga bao la pili kwa Manchester United dakika ya 84 ambalo ni la utata na mithili ya tamthilia ya Ze Komedi na kuwafanya Wachezaji wa Tottenham wamzonge Refa Mark Clattenburg ambae hakutetereka kwenye uamuzi wake.
Mkasa huo ulianza pale Nani alipoangushwa ndani ya boksi na Difenda Kaboul na akiwa chini Nani alikuwa akidai penati huku akiugusa mpira kwa mkono na Kipa Heurelho Gomes akautokea na kuudaka lakini Refa Clattenburg hakupuliza filimbi.
Kipa Gomes akidhani imetolewa faulo ndipo aliuweka mpira chini na ndipo Nani akainuka na kwenda kufunga goli na Refa Clattenburg akatoa ishara weka kati, ni goli.
Bao la kwanza la Manchester United lilifungwa bila utata dakika ya 31 na Nemanja Vidic kufuatia frikiki ya Nani.
Kwa ushindi wa leo Manchester United wapo nafasi ya pili wakifungana na Arsenal wote wakiwa na pointi 20.
Chelsea ndie yuko juu akiwa na pointi 25.
Vikosi vilivyoanza:
Man United: Van der Sar, Rafael Da Silva, Ferdinand, Vidic, Evra, Nani, Fletcher, Carrick, Park, Hernandez, Berbatov
Akiba: Kuszczak, Brown, Smalling, Scholes, O'Shea, Obertan, Bebe.
Tottenham: Gomes, Hutton, Kaboul, Gallas, Assou-Ekotto, Lennon, Modric, Jenas, Bale, Van der Vaart, Keane.
Akiba: Cudicini, Pavlyuchenko, Palacios, Crouch, Bassong, Kranjcar, Sandro.

No comments:

Post a Comment