Sunday, October 31, 2010


Ikiwa imebaki siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu 2010, mgombea wa urais kupitia tiketi ya Chama cha Chadema, Dk. Willbroad Peter Slaa amejibu swali la mpiga kura aliyetaka kujua kinachoendelea katika ile ishu yake na mchumba’ke, Josephine Mshumbusi na kudai kuwa suala hilo waachiwe wao wenyewe.

Akijibu swali hilo katika laivu intavyu na Kituo cha Radio Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast, Jumatano wiki hii, ‘Dokta’ Slaa alisema kuwa suala la ndoa ni mkataba na siyo jambo la kujadiliwa hadharani hivyo kuomba jambo hilo kubaki mikononi mwake na Josephine.
Dk. Willbroad Peter Slaa.
“Ndoa ni mkataba kati ya mwanaume na mwanamke, niachieni mchumba wangu tufuate taratibu za dini zetu,” alisema Dokta Slaa na kuongeza:

“Hakuna tatizo lolote la ndoa, siyo suala la kujadili hadharani kwa kuwa lilikwenda mahakamani na huko lilikwama, mbona baadhi ya magazeti yaliyokuwa yakiandika hayakuandika tena?”

Mwanzoni mwa kampeni, Dokta Slaa alitumiwa kumpora Josephine aliyekuwa mke wa ndoa wa Aminiel Mahimbo na kusababisha kuibuka kwa gogoro zito lililoishia kupelekana mahakamani.
Josephene Mushumbushi.
Baadaye suala hilo lilishauriwa kwenda kwenye tume ya usuluhishi, hivyo likabaki mikononi mwa tume na wahusika.

1 comment: