Sunday, October 31, 2010

JK akipiga kura yake katika kituo cha kupigia kura Shule ya Msingi Msoga, kata ya Msoga,Chalinze leo asubuhi.
JK akionyesha wino uliopo katika kidole chake ikiwa ni ishara ya kuonyesha kuwa keshapiga kura leo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi Msoga iliopo Chalinze leo asubuhi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein akipiga kura kwenye kituo cha Uchaguzi Shule ya Msingi Oyesterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi
PICHA:WADAU WA CHALINZE

KITUO HAKINA WAPIGA KURA, MAKARANI WANAKULA CHAPATI TU!

Kituo cha kupigia kura cha Manzese kwa Bakhresa kimekutwa na mtandao huu muda wa saa sita mchana hakina watu hivyo makarani wake kupata wasaa wa kunywa chai na chapati kama wanavyoonekana pichani. Ilitarajiwa eneo hilo kuwa na misuru mirefu ya watu kutokana na mikutano yake, ya kampeni ya kina Slaa na JK iliyofanyika eneo hilo kuvuta watu wengi!

KASKAZINI YAONGOZA KWA VURUGU UCHAGUZI


Kanda ya Kaskazini, hasa Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Mara ndiyo inayoongoza kwa vurugu za Uchaguzi Mkuu 2010 tofauti na mingine ya Tanzania Bara.

Kisiwa cha Pemba, Zanzibar ambacho uchaguzi uliopita kiliweka rekodi ya ghasia nyingi za uchaguzi, mwaka huu ni amani, hivyo mikoa hiyo kutia fora.

Kwa mujibu wa utafiti wa gazeti hili, majimbo mawili ya Kilimanjaro, moja la Arusha na lingine Mara ndiyo yamekuwa yakiripotiwa kwa wafuasi wake kutwangana.

Katika orodha hiyo, Mkoa wa Iringa kupitia jimbo lake la Iringa Mjini, limeripotiwa pia wafuasi wa CHADEMA na CCM kutwangana.

Aidha, uchunguzi unaonesha kuwa ni vyama viwili tu ambavyo vimeripotiwa kwa vurugu ambavyo ni CCM na CHADEMA, wakati miaka iliyopita ghasia ziliripotiwa baina ya CCM na CUF.

Katika uchunguzi huo, Jimbo la Moshi Mjini ghasia ziliripotiwa mara kadhaa kati ya Mgombea Ubunge wa CHADEMA, Philemon Ndesamburo ‘Ndesa Pesa’ na Yule wa CCM, Justine Salakana kiasi cha polisi kuwawekea ulinzi maalum.

Hai, ni hivi juzi tu, Mgombea Ubunge wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipigwa mawe katika msafara wake, walengaji wa shabaha wakitajwa ni wafuasi wa CCM.

Jimbo la Tarime, Mara ambalo mwaka huu lilionekana kupoa tofauti na miaka iliyopita, nalo tayari limeanza kufukuta baina wanachama wa CHADEMA dhidi ya CCM kwa upande mmoja na mwingine CUF dhidi ya CHADEMA.

Jimbo la Arusha Mjini, wafuasi wa mgombe ubunge wa CHADEMA, Godless Lema na Dk. Batilda Buriani (CCM), hapotoshi kutokana na fujo zinaendelea.

Jumanne ya wiki, mkutano wa Lema, uliokuwa unafanyika kwenye Kata ya Mateves ulivunjika kutokana na kile kilichoelezwa kwamba wafuasi wa CHADEMA walikamata gari la Ikulu lililokuwa linafanya kazi za kampeni za CCM.

Ikiwa imebaki siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu 2010, mgombea wa urais kupitia tiketi ya Chama cha Chadema, Dk. Willbroad Peter Slaa amejibu swali la mpiga kura aliyetaka kujua kinachoendelea katika ile ishu yake na mchumba’ke, Josephine Mshumbusi na kudai kuwa suala hilo waachiwe wao wenyewe.

Akijibu swali hilo katika laivu intavyu na Kituo cha Radio Clouds FM kwenye kipindi cha Power Breakfast, Jumatano wiki hii, ‘Dokta’ Slaa alisema kuwa suala la ndoa ni mkataba na siyo jambo la kujadiliwa hadharani hivyo kuomba jambo hilo kubaki mikononi mwake na Josephine.
Dk. Willbroad Peter Slaa.
“Ndoa ni mkataba kati ya mwanaume na mwanamke, niachieni mchumba wangu tufuate taratibu za dini zetu,” alisema Dokta Slaa na kuongeza:

“Hakuna tatizo lolote la ndoa, siyo suala la kujadili hadharani kwa kuwa lilikwenda mahakamani na huko lilikwama, mbona baadhi ya magazeti yaliyokuwa yakiandika hayakuandika tena?”

Mwanzoni mwa kampeni, Dokta Slaa alitumiwa kumpora Josephine aliyekuwa mke wa ndoa wa Aminiel Mahimbo na kusababisha kuibuka kwa gogoro zito lililoishia kupelekana mahakamani.
Josephene Mushumbushi.
Baadaye suala hilo lilishauriwa kwenda kwenye tume ya usuluhishi, hivyo likabaki mikononi mwa tume na wahusika.

Na Herman Mwampyate
MNAJIMU na Mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein amesisitiza kwamba utabiri wake uko pale pale na kwamba Uchaguzi Mkuu mwaka huu hautafanyika kwa mujibu wa nyota.

Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake juzi (Jumatano), Sheikh Yahya alisema kwa kawaida akishatabiri kitu kinachofuata ni kusubiri na siyo kazi yake kuhakikisha kwamba kile alichotabiri kinatokea.

“Kwa kawaida mtabiri anapotabiri siyo kazi yake tena kuhakikisha kile alichokitabiri kinatokea, kwa hiyo watu wasubiri tu waone kwa sababu siku bado zipo kabla ya uchaguzi,” alisema.
Sheikh Yahya Hussein.
Alisema anapotabiri huwa hatumii uchawi ‘ndumba’ kama wengi wanavyofikiri, isipokuwa anatumia hesabu za kinyota na wala siyo utashi wake au wa watu anaowatabiria.

“Mwaka 2005 nilitabiri kwamba Rais (wa wakati ule) Benjamin William Mkapa ataongezewa muda wa kutawala zaidi ya ule wa kikatiba, watu waliona kuwa ni kitu ambacho hakiwezekani, lakini alipoongezewa kutokana na tatizo la kifo cha mgombea mmoja, walinipongeza kwa kuona ni maajabu,” alisema.

Akifafanua zaidi alisema mwaka huo aliona kinyota kuwa kuna mgombea atapoteza maisha lakini kistaarabu hukuweza kusema hivyo na akaongeza kwamba hata uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2000 alitabiri kuwa utarudiwa watu walipinga lakini ukarudiwa kweli.
“Wakati ule niliposema CCM na CUF siku za usoni wataunda serikali moja, nilikuwa sieleweki kabisa, hasa kutokana na jinsi vyama hivyo vilivyokuwa na uhasama mkubwa, lakini mimi niliwaambia siyo ninayefanya hayo, kwani ni mambo ya astrology (Unajimu),” alisema Sheikh Yahya.

Akifafanua zaidi, Sheikh Yahya alisema kwamba yeye akishatabiri si kazi yake tena kujua lini kitu alichokisema kitatokea, isipokuwa huwa anawaomba wananchi wasubiri matokeo.

Hata hivyo, alisema yeye bado anaamini elimu yake ya kinyota kwa sababu katika uchaguzi wa mwaka huu kuna watu kadhaa waliojitokeza kwa nia ya kutaka kuusimamisha kwa sababu mbalimbali japokuwa hawakufanikiwa, kitu ambacho kinaashiria kwamba elimu ya nyota huwa haisemi uongo kwa kuwa haijawahi kutokea hivyo miaka ya nyuma.

Boti

October 31, 2010
Boti ya kifahari ikipita mbele ya soko kuu la Ferry juzi, Haikujulikana mara moja boti hoi inamilikiwa na nani na wala ilikuwa ikielekea wapi. ingawa habari zinasema kuwa Boti hii inamilikiwa na Bakhresa na itakuwa ikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Leave a Comment » | Michezo

Saturday, October 30, 2010

RATIBA:
Jumapili, 31 Oktoba 2010
[Saa 8 mchana]
Aston Villa v Birmingham
[Saa 9 na nusu mchana]
Newcastle v Sunderland
[Saa 12 jioni]
Bolton v Liverpool
Jumatatu, 1 Novemba 2010
[Saa 5 usiku]
Blackpool v West Brom

Ligi Kuu England

Man United 2 Spurs 0, Nani afunga goli la ‘Ze Komedi’

Jumamosi, 30 Oktoba 2010 21:56
ChapishaToleo la kuchapisha
MAN_U_LOGONani alifunga bao la pili kwa Manchester United dakika ya 84 ambalo ni la utata na mithili ya tamthilia ya Ze Komedi na kuwafanya Wachezaji wa Tottenham wamzonge Refa Mark Clattenburg ambae hakutetereka kwenye uamuzi wake.
Mkasa huo ulianza pale Nani alipoangushwa ndani ya boksi na Difenda Kaboul na akiwa chini Nani alikuwa akidai penati huku akiugusa mpira kwa mkono na Kipa Heurelho Gomes akautokea na kuudaka lakini Refa Clattenburg hakupuliza filimbi.
Kipa Gomes akidhani imetolewa faulo ndipo aliuweka mpira chini na ndipo Nani akainuka na kwenda kufunga goli na Refa Clattenburg akatoa ishara weka kati, ni goli.
Bao la kwanza la Manchester United lilifungwa bila utata dakika ya 31 na Nemanja Vidic kufuatia frikiki ya Nani.
Kwa ushindi wa leo Manchester United wapo nafasi ya pili wakifungana na Arsenal wote wakiwa na pointi 20.
Chelsea ndie yuko juu akiwa na pointi 25.
Vikosi vilivyoanza:
Man United: Van der Sar, Rafael Da Silva, Ferdinand, Vidic, Evra, Nani, Fletcher, Carrick, Park, Hernandez, Berbatov
Akiba: Kuszczak, Brown, Smalling, Scholes, O'Shea, Obertan, Bebe.
Tottenham: Gomes, Hutton, Kaboul, Gallas, Assou-Ekotto, Lennon, Modric, Jenas, Bale, Van der Vaart, Keane.
Akiba: Cudicini, Pavlyuchenko, Palacios, Crouch, Bassong, Kranjcar, Sandro.

Sunday, October 24, 2010

Hi Guys

Nimerudi tena kwa kasi na nguvu mpya,ni mchakato wa kampeni majimboni ndio yamenifanya kijana wenu niwe busy sana ila nimewaandalia mambo motomoto na mkae mkao wa kula vitu vitamuu.